KATIKA kuelekea Uchanguzi Mkuu mwaka huu unaotarajia
kufanyika Oktoba, vijana wengi wamejitokeza kuwania majimbo mbalimbali
na katika Jimbo la Bagamoyo ambalo linashikiliwa na Mbunge Shukuru
Kawambwa kwa miaka 10 mfululizo, tayari kada wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mathew Yungwe amejitokeza kuwania kiti hicho.
 |
| Mtangaza nia akisiliza kwa makini. |
Akiomba ridhaa ya kulitumikia jimbo hilo kwa wananchi wa eneo hilo
katika Ukumbi wa Macho Kodo iliyopo wilayani humo, Yungwe amesema iwapo
atapata nafasi ya kuwa mbunge, vipaumbele vyake ni katika sekta ya afya,
uchumi na mawasiliano, sekta ambazo zimekuwa na misukosuko kwa muda
mrefu.
“Nitahakikisha kila Kikundi cha Saccos kinatoa asilimia tano ya faidi
yao kwa ajili ya wazee, suala la migogoro ya ardhi inapungua na pia
nitaweka misingi na kuboresha Soko la Samaki ili vijana wenzangu wapate
ajili ya kudumu kwa kuuza bidhaa hiyo ndani ya nje ya Bagamoyo,” alisema
na kutambulisha kauli mbiu yake ni ‘Fikiria Tofauti Kwa Maendeleo
Endelevu ya Bagamoyo’.
(Picha na Habari GPL/Deogratius Mongela )
No comments:
Post a Comment