Jeshi la Marekani linasema kuwa
mmoja viongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, ameuwaua katika
shambulio la angani lililotekelezwa na ndege za kijeshi za Marekani
Nchini Syria.
Al Fahdli anajulikana kama mtu muhimu katika Khorasan ambao ni mtandao muhumu kwa kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo lilikuwa likitumwa kutokea Pakistani na Syria kwa ajili ya kufanya mashambulizi ya kigaidi kwa nchi za magharibi.
Mfadhili huyo mkubwa wa kundi la kigaidi amekuwa akitafutwa na marekani kwa mara kadhaa ambapo Marekani ilitangaza kitita cha dola milioni saba kwa yoyote atakayefanikishwa kuauwa kwake.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon anasema Al Fahdli alikuwa miongoni mwa watu wachache wanaoaminiwa na kiongozi wa Al Qaeda ambaye pia aliwahi kupewa taarifa za kutokea kwa shambulio la kigaidi septemba 11 huko Marekani. Taarifa za kifo chache zilisambazwa tangu mwaka jana lakini ni sasa imethibitishwa kuwa Al Fahdli ameuawa Julai 8 mwaka huu huko Syria.
No comments:
Post a Comment