| Hissene Habre |
Kesi hiyo inafuatia miaka 25 ya kampeni za kumfikisha mbele ya sheria. Wengi miongoni mwa watu wanaodaiwa kuwa waathirika wa uhalifu uliotekelezwa na Bwana Habre' wamekua wakitoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi yake tangu alipopinduliwa mamlakani na kukimbilia uhamisho nchini Senegal 1990.
Mnamo mwaka 2005 mahakama ya Ubelgiji iliytoa kibali cha kumkamata, ikidai kuwa na haki ya kimataifa ya kufanya hivyo , lakini baada ya mazungumzo na Umoja wa Afrika , AU iliiomba Senegal kuendesha kesi dhidi Bwana Habre " kwa niaba ya Afrika ".
No comments:
Post a Comment