| Jack Warner |
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Trinidad na Tobago ametoa kibali juu ya kesi iliyofunguliwa na Marekani
dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA
Jack Warner.
Warner pamoja na maofisa wengine kumi na watatu wa sasa na wa zamani wa FIFA walipewa mashitaka na mamlaka ya Marekani tokea mwezi Mei mwaka huu.
Warner amekanusha mashitaka yanayomkabili. Juma lililopita, serikali ya Switzerland ilithibitisha kuachiliwa kwa Kiongozi mwingine wa FIFA Eugenio Figueredo kutoka Uruguay. Figueredo alikamatwa mwezi Mei alipokwenda nchini humo kwa shughuli za kikazi za FIFA.
No comments:
Post a Comment