Akaunti hiyo itaratibiwa na Benki kuu ya nchini humo na inakadiriwa kuwa Benki za biashara zitapoteza kiasi cha dola bilioni kumi pesa zitakapohamishwa.
Wizara zitazoshindwa kutimiza agizo hilo zitawekewa vikwazo. Rais Muhamadu Buhari, aliyetoa agizo la kufunga akaunti mbalimbali za benki amesema anaamini maafisa wa serikali wameiba kiasi cha dola bilioni 150 kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Mwandishi wa BBC jijini Abuja amesema utekelezaji wa hatua ya ''akaunti moja'' umewezesha jimbo la kaduna kubaini kiasi cha dola milioni 13 ambazo awali zilikuwa hazifahamiki kama zilikuwepo.
No comments:
Post a Comment