Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani
Papa Francis amewasili nchini Marekani katika siku ya kwanza ya ziara ya
kiistoria nchini humo ambapo amelakiwa na Rais wa nchi hiyo Barack
Obama.
Huku Wamarekani ikiwa na zaidi ya waumini wa Katoliki wapatao milioni sabini ziara hiyo ya papa inaoneka kuwa tukio kubwa nchini humo.
Kiongozi huyo wa kidini ambaye anaitembelea Marekani kwa mara ya kwanza atafanya ziara na kuendesha ibada katika miji ya Washington, New York na Philadelphia.
Wakati papa Francis akiondoka nchini Cuba papa Francis aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio muumini wa mlengo wa kushotoa kama wengi wanavyomtafsiri.
Papa alisema hataongelea suala la vikwazo vya biashara kati ya Cuba na Marekani,licha ya kuchukua nafasi muhimu katika mazungumzo ambayo yamesababisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kurejeshwa mapema mwaka huu.
No comments:
Post a Comment