Pages

Monday, 21 September 2015

Treni ya umeme yaanza kutumika Ethiopia

Ethiopia imezindua rasmi usafiri za treni ya umeme ya kubeba abiria mijini, ambayo ndiyo ya kwanza katika nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Treni Ethiopia

Treni hiyo itatumika katika mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa kwenye reli ya umbali wa kilomita 34, ikipita mji huo kutoka kaskazini kwenda kusini.

Mradi huo umegharimu $470 milioni (£300 milioni, ukifadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Uchina. Mamlaka nchini humo zimesema mradi huo, utafanyakazi kwa saa 16 na unatarajiwa kupunguza msongamano wa magari barabarani, huku watu milioni moja wakitarajiwa kuutumia kila siku.

Nauli inatarajiwa kuwa chini ya nusu dola kwa kila safari. Mwandishi wa BBC mjini humo Emmanuel Igunza, aliyehudhuria uzinduzi wa treni hiyo, anasema raia walijawa na msisimko mkubwa na kila mmoja alitaka kuwa wa kwanza kuiabiri.

No comments:

Post a Comment