Memphis Depay alianza kuifungia timu yake bao la kwanza kabla ya Héctor Moreno wa PSV kusawazisha kisha Luciano Narsingh akafunga bao la ushindi.
Man City nao wakiwa katika dimba lao la Etihad walikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa vibibi vizee vya Turin Juventus mabao ya Juve yakifungwa na Álvaro Morata na Mario Mandzukic huku bao la kujifunga la beki Giorgio Chiellini, likiwapa Man City bao moja.
Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameshinda kwa kishindo kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk, Cristiano Ronaldo akifunga hat trick na Karim Benzema akifunga bao moja.
Matokeo mengine ya michuano hii ni:
PSG 2 – 0 Malmö FF
VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA
Benfica 2 – 0 FC Astana
Galatasaray 0 – 2 Atletico Madrid
Sevilla 3 – 0 Borussia Mönchengladbach
No comments:
Post a Comment