Pages

Friday, 25 September 2015

Waziri Celina Kombani afariki dunia

Celina Kombani
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma nchini Tanzania Celina Kombani amefariki dunia.

Waziri Kombani ambaye pia alikuwa ni mbunge wa jimbo la Ulanga mashariki, amefariki jana Septemba 24, wakati akipata matibabu nchini India.


Alizaliwa Juni 19, 1959, na alikuwa mbunge kupitia chama tawala CCM. Rais Jakaya Kikwete ni miongoni wa waliotuma risala za rambirambi kumuomboleza waziri huyo.
"Ndugu yetu na mtumishi wa wananchi, Bi Celina Kombani ametangulia mbele za haki. Moyo wangu uko pamoja na familia yake wakat i huu wa majonzi," amesema kupitia akaunti yake ya Twitter.

No comments:

Post a Comment