Timu ya taifa ya England imeshinda
mchezo wake wa kumi katika michezo kumi ya kusaka tiketi ya kushiri
katika michuano ya Euro mwaka 2016 huko nchini Ufaransa.
England
ambao tayari wamefuzu kushirikia michuano ijayo ya ulaya imewachapa
Lithuania kwa mabao 3-0 kwa mabao ya Ross Barkley golikipa Giedrius
Arlauskis akijifunga bao la pili na Alex Oxlade-Chamberlain akfunga bao
la ushindi.
Hispania nao wakawachapa Ukraine kwa bao 1-0 bao pekee la Hispania likifungwa na Pérez Martínez katika dakika ya 21 ya mchezo.
Matokeo mengine ya michezo hiyo ya kufuzu kwa michuano ya ulaya
Belarus 0 – 0 Macedonia
Luxembourg 2 – 4 Slovakia
Estonia 0 – 1 Switzerland
San Marino 0 – 2 Slovenia
Austria 3 – 0 Liechtenstein
Russia 2 – 0 Montenegro
Sweden 2 – 0 Moldova
No comments:
Post a Comment