| Riek Machar |
Makamu wa rais wa zamani wa Sudan
Kusini, Riek Machar, anasema kuwa hajui ni lini atarejea nchini humo na
kuendelea na kazi yake.
Lakini Bwana Machar anasema kwamba kurejea kwake kunategemea hakikisho la usalama.
Anasema sio lazima amuamini Rais Salva Kiir, ili kufanya kazi naye, lakini akaongeza kuwa uamuzi wa hivi majuzi wa kubadilisha mipaka ya taifa hilo unakiuka makubaliano ya amani.
Alikosana na Rais Salva Kiir muda mfupi baada ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo mwaka wa 2011.
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalianza na Bw Machar akaukimbia mji mkuu Juba, mwezi Desemba ya mwaka huo.
No comments:
Post a Comment