John Pombe Magufuli sasa ndiye rais
mpya wa taifa la Tanzania baada ya kuapishwa rasmi kufuatia ushindi wake
wa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu uliopita.
| Rais Magufuli |
| Magufuli |
Amesema kuwa licha ya kwamba alipata changomoto kubwa kutoka kwa upinzani alioupata amepata funzo kubwa kutoka kwao.
| Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. |
Awali aliyekuwa rais wa taifa hilo Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili katika uwanja wa sherehe hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu waliomkaribisha kwa vifijo na nderemo.
Kikwete aliuzunguka uwanja huo akiwapungia mkono wa kwaheri raia hao waliojaa uwanja huo.Baadaye Bendera ya utawala wake ilishushwa huku rais mpya John Magufuli akiapishwa na makamu wake wa rais Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment