Pages

Tuesday, 3 November 2015

Wajua picha hii ilitoka wapi?

Mvulana

Picha hii ya mvulana anayeonekana kujiuliza maswali si haba akilini mwake akiwa na Mzungu imesambazwa mara nyingi sana mtandaoni.

Wengi wamekuwa wakiitumia kukejeli vyombo vya habari, mataifa na mashirika ya kutoa misaada kutoka Magharibi kwa mtazamo wao kuhusu Afrika. Kunao wanaoitumia hata hivyo kuuliza maswali ya kijumla tu.

Lakini je, wajua picha hii ilitoka wapi? Mvulana huyu ni nani?



Picha hii ilianza kuenea sana mtandaoni baada ya kupakiwa kwenye tovuti ya Reddit miaka mitatu iliyopita na mwanamume kutok Texas, Marekani aliyevutiwa nayo baada ya kuiona kwenye ukurasa wa Facebook wa rafiki yake.

Mwanamke aliye kwenye picha hiyo ni Heena Pranav, daktari mwenye umri wa miaka 28 anayeishi Chicago.

Mwaka 2012, alipokuwa mwanafunzi, alizuru mji wa Gulu, kaskazini mwa Uganda kusaidia kwenye mradi wa kuwasaidia wanawake walioathiriwa na vita vya wapiganaji wa Lords Resistance Army. Mradi huo ulisimamiwa na shirika laPros for Africa, linaloongozwa na mtawa Mkatoliki, Rosemary Nyirumbe.

Picha hiyo haikuhusiana na mradi huo na Pranav, akizungumza na BBC Trending radio, amesema alikutana na mvulana huyo sokoni na anakadiria alikuwa na umri wa miaka miwili au mitatu.

"Nilikuwa na wanafunzi wengine wakati huo, na tulikuwa tunapiga gumzo na nikaona mvulana mdogo, aliyenivutia sana,” Pranav alisema.

No comments:

Post a Comment