Wapalestina 2 wauawa na Waisraeli
Maafisa wa afya wa Palestina
wanasema wapalestina wawili wameuawa baada ya vikosi vya Israeli
kufyatua risasi katika ukingo wa Magharibi.
Wapalestina wengine watatu wamejuriwa. Duru
za kijeshi za Israeli zasema wanajeshi wake wamejeruhiwa katika eneo la
Qalandia karibu na kambi ya wakimbizi wa kipalestina ya huko Ramallah.
Wanajeshi
hao wa Israeli walikabiliwa na upinzani walipokuwa wakibomoa nyumba ya
mpalestina mmoja anaeshukiwa kumuua mu-Israeli mwezi juni.
Mapigano hayo ndiyo ya hivi punde zaidi kutokea baina ya Waisraeli na Wapalestina.
Hadi kufikia sasa waisraeli 13 wamepoteza maisha yao huku zaidi ya Wapalestina 80 wakipoteza maisha.
No comments:
Post a Comment