Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi.Regina Chonjo ametangaza hali ya hatari
katika wilaya hiyo baada ya kupokea tarifa za kiintelijensia za kuwepo
matukio ya uhalifu yanayoshabihiyana na vitendo vya ugaidi katika maeneo
tofauti ya wilaya hiyo na hivyo kufuta vibali vyote vya mikusanyiko
isiyo ya lazima hadi itakapo tangazwa hali ya amani.
Mkuu wa wilaya Bi.Chonjo ametoa tarifa hiyo wakati wa wito wa dharura
kwa waandishi wa habari ambapo amewataka wananchi wote wa wilaya ya
Morogoro kutoa tarifa katika vyombo vya dola wanapoona watu
wasiowafahamu na matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani.
Aidha amewataka wamiliki wa vyumba za kulala wageni na kumbi za starehe
kuwa makini na wageni wanaoingia na kutoka huku akiwataka wenyeviti wa
vjiji,mitaa pamoja na watendaji wote kufanya jitihada za kuwatambua
wageni wote walioko katika maeneo yao.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa wilaya Morogoro wameomba Jeshi la
Polisi kuimarisha ulinzi katika kituo cha mabasi cha Msamvu pamoja na
maeneo ya sokoni kwani ndiyo maeneo yenye mikusanyiko ambayo haiwezi
kuzuiliwa.
Chanzo: ITV