PICTURE: Mwanzilishi wa Facebook(Mark Zuckerberg) Alivyotembelea Nigeria
MWANZILISHI na mmiliki wa mtandao maarufu duniani wa Facebook,
Mark Zuckerberg juzi Jumanne alianza ziara yake ya siku mbili nchini
Nigeria, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwa nchi za Afrika, na kukutana
watu mbalimbali wakiwemo wasanii maarufu wa uigizaji filamu na muziki
nchini humo.