![]() |
Akizungumza na waandishi wa habari jana
Jumatano, jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda hiyo Kamanda Simon
Sirro alisema kuwa watu hao wamekamatwa katika operesheni inayoendelea
kufanywa na jeshi hilo maeneo ya Vikindu nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam.
“Operesheni inapata mafanikio makubwa
tangu ilipoanza na kwamba tumewakamata watu zaidi ya 20 maeneo ya
vikindu na Dar es Salaam wakihusishwa na matukio mbalimbali ikiwemo lile
la mauaji, ” amesema.
Aidha, Kamanda Sirro amewashukuru
viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuaghirisha
operesheni Ukuta waliyoipanga kuifanya kesho.
“Niwapongeze kwa maamuzi ya busara
waliyofanya maana ni ya kizalendo, niwahakikishie tu kwamba Dar es
Salaam iko salama na pia niwatoe hofu wananchi kuwa wasiogope watakapo
waona askari barabarani sababu kazi yao ni kufanya doria ili jiji liwe
salama, ” amesema.
Pia amesema Viongozi waandamizi wa
Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe na Edward
Lowassa waliotakiwa kuripoti kesho Katika kituo hicho, wanatakiwa
kuripoti siku ya jumanne ya wiki ijayo.Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam limesema limewakamata zaidi ya watu 20 ambao kati yao
wanahusishwa na tukio la mauaji ya askari polisi 4 lililotokea siku za
hivi karibuni maeneo ya Mbande, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda hiyo Kamanda Simon Sirro amesema
kuwa watu hao wamekamatwa katika operesheni inayoendelea kufanywa na
jeshi hilo maeneo ya Vikindu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
“Operesheni inapata mafanikio makubwa
tangu ilipoanza na kwamba tumewakamata watu zaidi ya 20 maeneo ya
vikindu na Dar es Salaam wakihusishwa na matukio mbalimbali ikiwemo lile
la mauaji, ” amesema.
Aidha, Kamanda Sirro amewashukuru
viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuaghirisha
operesheni Ukuta waliyoipanga kuifanya kesho.
“Niwapongeze kwa maamuzi ya busara
waliyofanya maana ni ya kizalendo, niwahakikishie tu kwamba Dar es
Salaam iko salama na pia niwatoe hofu wananchi kuwa wasiogope watakapo
waona askari barabarani sababu kazi yao ni kufanya doria ili jiji liwe
salama, ” amesema.
Pia amesema Viongozi waandamizi wa
Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe na Edward
Lowassa waliotakiwa kuripoti kesho Katika kituo hicho, wanatakiwa
kuripoti siku ya jumanne ya wiki ijayo.