Pages

Wednesday, 8 April 2015

kile ambacho Irene Uwoya anakumbuka kuhusu Marehemu Steven Kanumba

Leo ni siku ambayo mashujaa wawili wanakumbukwa TZ.. Kwanza ni hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa Z’bar.. mwingine ni muigizaji nyota wa Bongo Movie, Steven Kanumba.SONY DSC


Irene Uwoya ni mmoja wa wasanii ambao wamefanya sana kazi na Marehemu Kanumba, hiki ameshea na sisi kwenye kumbukumbu hii ya Kanumba;
Kiukweli nakumbuka mambo mengi sana.. Kwa sababu Steve kwangu mimi alikuwa mtu muhimu sana amenifundisha vitu vingi sana.. isitoshe Steve nilikuwa namjua kabla sijaanza kuingia kwenye sanaa nakumbuka vitu vingi kweli.. alikuwa mshkaji wangu sana mpaka nimeingia kwenye sanaa amenionesha njia vitu vingi tu tumefanya
Kinachoniumiza zaidi kuna mipango tu mingi ambayo tulikuwa tumepanga na yeye kabla hajafariki.. siku chache kabla hajafariki tulikuwa wote tumekaa tumekunywa.. tumeongea vitu vingi sana vya maisha na vya maendeleo kwa ajili ya tasnia.. baada ya kama siku mbili nikasikia hiyo. Tarehe ya leo inanikumbusha sana marehemu Steve, kiufupi siipendi siku ya leo.“– Irene Uwoya.

No comments:

Post a Comment