Ni
kama utaniuliza picha gani iliyovunja internet au kushikilia headlines
za internet kwa saa kadhaa April 7 2015 Tanzania, jibu lake litakua ni
hii picha ya msanii wa bongofleva Nay wa Mitego na mwigizaji wa bongo movie Shamsa Ford.
Majibu ya Nay wa Mitego kuhusu hii picha ni
kwamba ni movie ndio inachezwa ambapo kama kweli ni movie basi hii ndio
itakua movie ya kwanza sisi tulio wengi kumuona Nay wa Mitego.
Wawili
hawa wametajwa kuwepo mapenzini kwa kiasi kikubwa siku za karibuni
ambapo Shamsa ambaye aliingia kwenye headlines za Magazeti baada ya
kuachana na mume wake, amepost picha mbili ndani ya siku tano zilizopita
akiwa kwenye Gym ya Nay wa Mitego.
Kwenye hii picha ya juu hakuandika chochote kama caption ila hii picha ya chini mrembo huyu aliandika >>> ‘On Set‘ yaani ni kwenye utengenezaji wa movie.Unataka kujua wenyewe watasema nini kwenye Interview na AyoTV na millardayo.com ? kaa karibu yangu mda wowote kutoka sasa nakudondoshea mtu wangu.
No comments:
Post a Comment