Kulikuwa na kaburi la muda,misalaba
na mishumaa vilivyowekwa katika viwanja vya mji mkuu wa Kenya ,Nairobi
ili kuwakumbuka wanafunzi waliouawa katika shambulio la chuo kikuu cha
Garissa ,shambulio ambalo lililotekelezwa na mwanamgambo aliyekuwa na
silaha kutoka katika kundi la Al Shabaab,mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wanafunzi waliouawa Garissa.
Picha
za waathirika wa shambulio hilo wapatao mia moja na arobaini na nane
ziliwekwa bayana katika ibada ya mkesha, katika maadhimisho ya
kuhitimisha maombolezo ya kitaifa nchini humo yaliyodumu kwa muda wa
siku tatu.
Waandaji wa mkesha huo waliwataka waombolezaji waliokuwa tayari
kuhudhuria ibada hiyo, kuvaa mavazi meusi,na pia kubeba maua ridi .
Mapema,wanachuo kutoka chuo cha Garissa waliandamana katika mji mkuu wa
Nairobi,huku wakiwa na ujumbe wenye kuitaka serikali ya Kenya kuimarisha
ulinzi nchini humo.
Garissa kwenyewe watu wapatao elfu mbili
walikusanyika katika mkutano wa hadhara ,nayo mahakama kuu mjini Nairobi
imetoa mwezi mmoja zaidi kwa polisi kuwahoji washukiwa sita wa tukio la
Garissa ambao wanashukiwa kuwapelekea silaha wauaji waliotekeleza tukio
lile.
No comments:
Post a Comment