Pages

Wednesday, 8 April 2015

Okwi awapa Yanga mambo matatu Waarabu wafe

Mshambuliaji hatari wa Simba, Emmanuel Okwi, amewapongeza wapinzani wake wakubwa, Yanga, baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini pia amewapa mambo matatu ili wawang’oe Waarabu.
OKWI

Yanga kwa sasa inatarajiwa kuvaana na Etoile du Sahel ya Tunisia kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora baada ya kuitupa nje Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2.Okwi aliwahi kuichezea Sahel na baadaye akaachana nayo kutokana na mgogoro ulioibuka na mpaka leo bado Simba hawajapewa fedha zao za usajili.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mganda huyo ambaye amewahi pia kuitumikia Yanga, alisema ni vizuri timu hiyo ya Jangwani ikapongezwa kwa hatua iliyofikia kwa kuwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi wamefanya kazi kubwa sana.
Lakini alisema kama watafuata mambo haya matatu watafuzu, wafanye mazoezi kwa nguvu, wawe na spidi na kujiandaa kwa mbinu zozote za ndani na nje ya uwanja kwa kuwa hao jamaa ni makini sana.Okwi alisema hata hivyo, Yanga wanatakiwa kuwa makini sana wakati wanapojiandaa na mchezo dhidi ya Sahel kwa kuwa ni timu bora Afrika.
“Naipongeza Yanga, lakini Yanga wanatakiwa kujiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Sahel kwa kuwa wale jamaa ni bora sana. Yanga wanatakiwa kubadilisha vitu vingi sana.“Wanatakiwa kufanya mazoezi ya nguvu huku wakiamini kuwa mechi iliyopo mbele yao ni kali, kama Yanga hawatakuwa makini, hakika hawatafuzu kwa kuwa hawa Waarabu ni watu makini sana, Yanga wanatakiwa kuwa na spidi na kujihami ndani na nje ya uwanja kwa kuwa Waarabu hawa wana mbinu sana.
“Nimewahi kuwatumikia wale jamaa, kwa hiyo nawafahamu vizuri sana,” alisema Okwi, ambaye timu yake kwa sasa ipo nafasi ya tatu kwenye ligi.Okwi kwa sasa ana mabao saba kwenye ligi kuu na amekuwa msaada mkubwa sana kwenye kikosi cha Simba kwa hapa kilipo.

No comments:

Post a Comment