Pages

Wednesday, 8 April 2015

Nani kuandaa fainali za Afcon 2017?

Nchi mojawapo kati ya Algeria, Gabon au Ghana zitachaguliwa Jumatano kuwa wenyeji wa michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 2017.
Wenyeji wa awali wa fainali hizo, Libya, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekwamisha shughuli za mpira, ilijitoa mwaka jana kuandaa mashindano hayo.
Kamati ya shirikisho la vyama vya soka barani Afrika, Caf, itaendesha uteuzi huo katika mkutano wake wa mwaka utakaofanyika mjini Cairo, Misri kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Caf pia itapanga ratiba ya kufuzu kwa fainali hizo, ambayo itazishirikisha pia nchi za Morocco na Tunisia.

Morocco ilifungiwa kushiriki katika fainali mbili mfululizo za shirikisho la Caf baada ya kushindwa kuandaa fainali za mwaka 2015 lakini walishinda kesi hiyo baada ya kukata rufaa katika mahakama ya michezo, CAS.
Tunisia imeondolewa adhabu ya kutoshiriki michuano ya shirikisho hilo baada ya kuomba radhi kwa kulishutumu shirikisho hilo kwa upendeleo.

No comments:

Post a Comment