Hali ya kutamauka imewakumba wengi waliothiriwa na tetemeko hilo,na wengine wameonesha malalamiko yao kwa kulumbana na polisi huko Kathmandu, mji mkuu wa taifa hilo.
Maelfu wameanza kuuhama mji huo mkuu.
Angalau sasa misaada ya bidhaa muhimu na huduma zimeanza kuwafikia mwaavijiji.
Wakati huo huo, Mwanamme aliyetolewa ndani ya vivusi katika hoteli iliyoporomoka mjini Kathmandu ameelezea jinsi aliweza kuishi kwa saa 82 kabla ya kuokolewa.
Rishi Khanal amesema alilazimika kunywa mkojoo wake wakati akisubiri kuokolewa.
Mguu wake alikwamba ndani ya vivusi lakini aliweza kuwasiliana na jamaa zake akitumia simu yake ya mkononi.
Hata hivyo hakumbuki hoteli alimokua. Aliokoewa na makundi ya wokozi kutoka Nepal na Ufaransa.
Zaidi ya watu elfu 5 wameuawa katika janga hilo la maporomoko ya ardhi huko Nepal.
No comments:
Post a Comment