Pages

Wednesday, 8 April 2015

Simba SC wajigamba kuendeleza vipigo Ligi Kuu Bara

Kikosi cha Simba baada ya juzi Jumatatu kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar, kimejigamba kuwa kitaendeleza ubabe wake kwenye ligi hiyo hadi mwisho.
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara.
  Simba ambayo kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 35, wikiendi hii inatarajiwa kupambana na Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku mchezo huo ukitarajiwa kuwa ni wa kisasi baada ya Simba kupoteza ule wa awali mkoani Tanga.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara, alisema kutokana na kuwa na hasira za kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mgambo, wataingia kwa lengo moja la kuibuka na ushindi na hali hiyo ndiyo itakuwa hadi mwisho wa ligi.
“Tunawatangazia wapinzani kuwa tutashusha vipigo mpaka ligi inaisha na tutaanza kulipiza kisasi wikiendi hii dhidi ya Mgambo kwani tuna hasira nao kutokana na kutufunga mchezo wa kwanza,” alisema Manara ambaye alitua Simba kwa mbwembwe akatangaza kuwa hatakuwa akizungumzia masuala ya kiufundi.

No comments:

Post a Comment