| Veronica |
Kim Little (Scotland and Seattle Reign) Mchezaji Scotland Little amekuwa na msimu mzuri katika ligi ya soka ya wanawake nchini Marekani ambapo anacheza kama mshambuliaji wa kiungo cha kati.Scotland aliongoza kwa mabao 16 mbali na kuchaguliwa kama mchezaji bora wa mwezi mara tatu mbali na kutajwa kuwa mchezaji bora katika msimu ambao timu yake Seattle,ilifuzu katika fainali kabla ya kupoteza mechi hiyo kwa kilabu ya Kansas.Ijapokuwa ana miaka 24,amecheza katika michuano ya kulipwa tangu mwaka 2006 na mwaka 2013 alichaguliwa kama mchezaji bora wa taji la PFA.Hatahivyo anaendelea kujiliwaza baada ya Scotland kushindwa kufaula kwa dimba la duniani nchini Canada 2015.Anasema:''Kufuatia kuwepo kwa wachezaji bora duniani na katika ligi ya Marekani kwangu mimi ni heshima kubwa kutambulika''.
Nadine Kessler (Germany and Wolfsburg) Ni nahodha wa timu bora barani Ulaya mbali na kuwa tegemeo la timu ya taifa ya Ujerumani, hakuna taji lolote katika soka ya wanawake ambalo Kessler hajashinda.Mchezaji huyo wa miaka 27 aliiongoza klabu ya Ujerumani Wolfsburg kushinda taji lao la pili la ligi ya wanawake barani Ulaya UEFA pamoja na taji la ligi ya Bundesliga msimu uliopita.Yote haya yalimwezesha kupata taji la FIFA la mchezaji bora wa mwaka 2015 duniani upande wa akina dada na kumrithi mchezaji mwenza wa Ujerumani Nadine Angerer.Hatahivyo kuna maswali mengi kuhusu iwapo majeraha mengi aliyonayo yatamruhusu kung'ara katika dimba la Canada mwaka huu.Anasema:''nilitaka kucheza soka ili kufanikiwa.lakini sidhani kwamba kitu kama hiki kinaweza kufanyika''.
Asisat Oshoala (Nigeria and Liverpool) Chipukizi Asisat Oshoala ni mchezaji wa kwanza kutoka Africa kushindana katika ligi ya soka ya wanawake.Akiwa na mataji ya mchezaji bora wa mwaka na mchezaji bora chipukizi mwaka huu,alijiunga na mabingwa wa ligi Liverpool kutoka Rivers Angels.Kwa jina la utani Seedorf,alikuwa mchezaji bora wa mchuano wa kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20 pamoja na kuisadia Nigeria kufuzu katika kombe la dunia nchini Canada.Vilevile alituzwa na rais wa Nigeria .Anasema:''Nahisi kukubalika. Niliweka juhudi kubwa mwaka uliopita lakini nimeshangazwa na uteuzi huu.Tuzo hii ni kitu kizuri sana katika soka ya wanawake, inaweza kutusaidia kwa kutoa motisha kwa mataifa mengine kuwasaidia wanawake wao na kuwachukulia sawa tu na wanaume''.
No comments:
Post a Comment