| Watu wawili wameripotiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mlipuko kwenye mji mkuu wa Afganistan Kabul. |
Haijabainika iwapo walikwepa shambulizi hilo au la. Lango hilo hutumika na maafisa wa kijeshi wa kigeni pekee yao.
Msemaji wa polisi nchini humo amaiambia BBC kuwa shambulizi hilo lilifanyika karibu na afisi za halmashauri za safari za ndege nchini humo zilizoko nje ya uwanja wa ndege.
Mtu aliyeshuhudia alilitaja shambulizi hilo kuwa la kujitoa mhanga. Shambulizi hilo linafanyika siku tatu baada ya mwanamgambo mmoja kuwaua watu 14 wakiwemo raia 9 wa kigeni mjini humo.
No comments:
Post a Comment