Taarifa zinasema kuwa wanamgambo wa
kundi la Islamic State wanasafirishwa kwenda barani Ulaya na walanguzi
wa binadamu wanaohudumu kwenye bahari ya Mediterranean.
Walanguzi wengine nchini Libya wanasema kuwa wanamgambo wa Islamic State huwaruhusu kuendelea na shughuli zao kwa malipo ya asilimia hamsini ya pesa wanazopata.
Mashirika ya mipaka barani ulaya mapema mwaka huu yalionya kuwa wapiganaji wa kigeni hutumia njia zisizokuwa za kawaida kuingia barani ulaya.
No comments:
Post a Comment