Afrika Kusini imeanzisha operesheni
ya kuwafurusha raia wa mataifa mengine ya Afrika kufuatia vurumai za
kibaguzi zilizoibuka dhidi ya wageni katika taifa hilo hivi majuzi.
Zaidi ya wageni 400 kutoka Msumbiji walikuwa katika kundi la kwanza kufukuzwa.
Afrika
Kusini imechukua hatua hiyo baada ya vurumai ya kibaguzi dhidi ya
wageni iliyopelekea watu saba raia wa kigeni kuuawa na wenyeji waliokuwa
wakilalama kuwa wamechukua nafasi zao za kazi.
Mapigano hayo ya kibaguzi yalitibuka katika miji ya Durban na
Johannesburg wenyeji walipoanza kuwavamia wageni pamoja na kuwapora mali
yao.
Serikali ya Msumbiji imeshangazwa na hatua hiyo ya kuwaondoa
raia wake kwa nguvu huku waziri wake wa maswala ya kigeni Oldemiro
Baloi akisema alikuwa anatarajia kufanya mazungumzo na mwenzake wa
Afrika Kusini.
Waziri huo alisema haelewi kwa
nini raia wa Msumbiji wanakamatwa na kuondolewa nchini humo kwa nguvu
ilhali swala hilo lilikuwa linashughulikiwa baina ya serikali hizo
mbili.
Hatua
hii ya serikali imewashangaza wengi hususan baada ya serikali kupewa
ilani ya mahakama dhidi ya kuwakamata na kuwafukuza wageni. Operesheni hiyo ya kuwakamata
wageni imekuwa ikiendeshwa majira ya alfajiri hasa katika mitaa duni ya
miji ya Durban na Johannesburg.
''Operesheni Fiela'' kama inavyofahamika ilipele

kea watu zaidi ya 889 kukamatwa.
Wanaharakati
wa haki za kibinadamu walikwenda mahakamani kupinga operesheni Fiela
wakisema inahalalisha vita vya kibaguzi vilivyo sababisha vifo vya watu
saba wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya Afrika.
Ulaya
No comments:
Post a Comment