Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu jaribio la mapinduzi la jumatano iliyopita.
Rais Nkurunziza akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Bujumbura alionya kuwa kuna tishio la shambulizi la kigaidi kutoka kwa kundi la waislamu kutoka Somalia wenye uhusiano na Al-Qaeda , Al Shabaab. Aliwaambia wandishi wa habari wa kimataifa kuwa tishio hilo la mashambulizi sio tu kwa taifa lake bali pia kwa Kenya na Uganda .
Duru kutoka kwa afisi za maswala ya usalama wanje katika serikali ya Marekani na vile vile maswala ya ndani ya serikali ya Uingereza zimekariri tishio hilo la Al Shaabab dhidi ya Burundi kufuatia mchango wake katika jeshi la umoja wa Afrika Amisom huko Somalia.
Marekani tayari imeagiza raia wake kuondoka nchini humo kufuatia tishio la shambulizi la kigaidi mbali na kuzorota kwa hali ya usalama.
No comments:
Post a Comment