Mlipuaji wa kujitolea muhanga
amejilipua ndani ya msikiti wa madhehebu ya Shia katika mkoa wa
mashariki wa taifa la Saudi Arabia na kusababisha madhara makubwa.
Kulingana na vyombo vya habari nchini humo. Mtu mmoja aliyeshuhudia alikiambia chombo cha habari cha Reuters kwamba kulikuwa na mlipuko mkubwa katika msikiti wa Imam Ali katika kijiji cha al-Qadeeh.
Watu wa dhehebu la Shia walio wachache wanaishi mkoa wa mashariki na kumekuwa na malalamishi ya washia wanaotaka kupewa haki zaidi. Hili ni shambulizi la kwanza lililotekelezwa katika msikiti wa Shia.
Tukio hilo linajiri huku muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ukiendeleza kampeni yake dhidi ya waasi wa kishia katika taifa jirani la Yemen. Taifa la Saudi Arabia pia limetishwa na Islamic state ambalo linalengwa na muungano wa kimataifa iwemo ufalme huo wa kisunni.
No comments:
Post a Comment