Viongozi Kaskazini mwa Kenya
wamesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al
Shaabab waliuvamia msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa kwa masaa
kadhaa.
Al Shaabab waliuteka msikiti mmoja katika
kaunti ya Garissa kwa muda na kuonya wenyeji dhidi ya kuisaidia serikali
ya Kenya na ujasusi
Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea mwituni. Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya Kenya.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom
Mwezi uliopita Al Shaabab walivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua watu 150 wengi wao wanafunzi. Kundi
hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na wafuasi nchini Kenya ambapo
limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya kuilazimisha serikali
ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni
miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom
ambao wanaisaidia serikali dhaifu ya Somalia kupigana na waasi wa Al
Shabaab.
Msikiti huo upo takriban kilomita 40km kutoka mji wa Garissa kulikotokea shambulizi la chuo kikuu mwezi uliopita.
Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao walikuwa wameandamana na wapiganaji takriban 40 waliojihami tayari kwa vita.
Mwandishi
wa BBC Abdullahi Abdi aliyeko mjini Nairobi anasema kuwa serikali ya
Kenya imeanza kujenga ua ilikuzuia mashambulizi kama hayo.
No comments:
Post a Comment