Australia imeonya kuwa haitawaruhusu wakimbizi wa jamii ya waislamu wa Rohingya waliowasili nchini humo kwa mashua kuishi.
Bwana Abbott anasema watu wanaotafuta uhamiaji wanafaa kufuata njia rasmi kuhusu uhamiaji.
''Haiwezekani eti kwa sababu umepanda mashua hafifu naambayo inavuja maji utatua nchi yeyote ya magharibi na unaanza maisha mapya !
''Ni wajibu wetu kila mmoja kuhakikisha kuwa tunakabiliana na ulanguzi wa watu'' aliongezea.
Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Malaysia na Indonesia wamo nchini Myanmar kwa ajili ya mazungumzo kuhusu tatizo hilo la wahamiaji.
Takriban watu 7,000 wanaaminika kuwa wamekwama baharini.
Wahamiaji hao wanajumuisha waislamu wa kabila la Rohingya wanaotoroka mateso pamoja na kuhangaishwa nchini Myanmar.
Wapo pia raia wa Bangladesh, ambao wanadhaniwa kuwa wahamiaji wanaotafuta hifadhi ya kiuchumi.
Malaysia pamoja na Indonesia zimesema kuwa zitatoa hifadhi ya muda kwa wale watakao wasili katika maeneo yao, lakini zinahitaji msaada kutoka jamii ya kimataifa kuwasaidia kuwapa makaazi.
No comments:
Post a Comment