Nia ya rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza kuwania muhula wa tatu imepata pigo baada ya ripoti kutoka
nchini humo kudai kuwa mwenyekiti msaidizi wa tume ya uchaguzi
ametoroka.
Afisa mmoja tume hiyo ya uchaguzi ameiambia redio moja
ya Ufaransa kuwa Spes Caritas Ndironkeye aliabiri ndege ijumaa na
haijulikani kama alijiuzulu au la.
Tume hiyo ya uchaguzi ina maafisa wakuu watano na inaweza kuendelea kuhudumu hata baada ya kuondoka kwa mmoja wao. Hata hivyo duru zinaelezea kuwa huenda afisa wa pili wa tume hiyo akajiondoa na hivyo kulemaza shughuli za tume hiyo.
Juma
lililopita kanisa katoliki nchini Burundi lilijiondoa kutoka kwa
harakati zozote za uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata siku moja tu kabla
ya umoja wa Ulaya kuondoa maafisa wake katika shughuli hizo za uchaguzi.
Umoja wa ulaya ulikuwa umetuma maafisa wa kucimamia na kuhakikisha kuwa uchaguzi huo ni wa huru na haki.
Taarifa hiyo imetokea wakati ikisalia wiki moja tu uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike nchini humo.
Kanisa
katoliki ni kiungo muhimu katika suala la amani na demokrasia nchini
Burundi tokea kuanzishwa mazungumzo ya amani ya Arusha mnamo miaka ya
tisini.
Haya yamearifiwa wakati maandamano dhidi muhula wa tatu wa
rais wa Burundi Pierre Nkurunziza yanaendelea kufanyika katika mitaa
kadhaa ya mji mkuu Bujumbura kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki wakati wa ghasia za maandamano,
Tangu
rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mwezi uliopita kuwa anapania
kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu, kinyume na katiba ya
Burundi.
Uchaguzi wa urais umepangiwa kufanyika Juni tarehe tano, huku ule wa urais ukiwa mwishoni mwa mwezi huo wa Juni
No comments:
Post a Comment