Wajumbe wa FIFA walioko nchini Uswiz
wameanza kumpigia kura rais mpya wa shirikisho hilo la soka duniani
huku shirikisho hilo likikabiliwa na shutuma za ufisadi.
Akifungua mkutano mkuu wa FIFA mjini Zurich, Bwana Mr Blatter alibainisha kuwa shirikisho hilo linakabiliwa na matatizo - lakini akatoa wito kwa wajumbe kushughulikia matatizo hayo kwa pamoja, Lakini kabla upigaji kura , mpinzani mkuu wa bwana Blatter.
Ali Bin al Hussein mwanamfale wa Jordan, aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kumuunga mkono -- kwa ajili ya kuboresha mchezo wa soka, Siku ya pili ya Kongamano hilo ndio inayomchagua Rais wa FIFA.
Awali kumekuwa shinikizo kwa FIFA kuhairisha kongamano hili na pia uchaguzi wa urais. hata hivyo maombi hayo yalifutiliwa mbali na inatarajiwa kuwa rais Sepp Blatter ataendelea mbele na uchaguzi ambao anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan.
Blatter aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wajumbe, katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo la kandanda duniani huko Zurich Uswisi.
Blatter ameahidi kukamilisha mabadiliko yatakayoirejeshea FIFA hadhi yake. Blatter anakabiliana na mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika leo.
Kwa upande wake mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan anasema kuwa yeye pekee yake ndiye aliye na nia ya kuleta mabadiliko ya kimsingi yatakayomaliza ufisadi na ulaji rushwa ndani ya FIFA.
Takriban wenyeviti wa mashirika 209 ya kandanda kote duniani wanakura moja kila mmoja .
Mwaandishi wa habari wa BBC, anasema kuwa Bwana Blatter anategemea uungwajji mkubwa kutoka kwa wajumbe wa mataifa ya Amerika, Afrika na Asia - ambao wanasema kuwa amefanya mengi katika kuboresha mchezo wa kandanda katika mataifa maskini.
No comments:
Post a Comment