Amisi Kalonda, afisa utawala wa kieneo Mashariki mwa Kongo amesema kuwa waasi wa harakati ya ADF-NALU wa Uganda ndio waliohusika na shambulio hilo lililotekelezwa katika eneo la Oicha umbali wa kilomita zisizopungua 20 kaskazini mwa mji wa Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini unaopakana na Uganda na Rwanda.
Martin Kobler, Mkuu wa Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) amesema kuwa hawezi kuvumilia mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya askari jeshi wa kofia buluu katika mkoa wa Beni.
Watu wanaosadikiwa kuwa waasi wa Uganda wa ADF wananyooshewa kidole kuhusika katika shambulio. Kundi la waasi la ADF linaendesha harakati zake katika eneo hilo tangu zaidi ya miaka 20 iliyopita. Mpaka sasa wanajeshi wawali wa Monusco ndio wanaripotiwa kuuawa na wengine wengi wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mmoja ambaye yuko katika hali ya maututi.
Shambulio hilo dhidi ya msafara wa magari ya MONUSCO limeendeshwa saa moja na nusu usiku. Zaidi ya wanajeshi ishirini wa MONUSCO kutoka Tanzania wamekua wakipiga doria kwenye barabara kuu inayotokea Beni kuelekea Mayimoya, karibu na kambi ya jeshi ya Mavivi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Shambulio hilo lilitokea kilomita zaidi ya kumi Kusini mwa mji wa Eringeti.
Wanajeshi hao wa kikosi cha Umoja wa Mataifa wamekua wakipiga doria peke yao, kwani tangu mwezi Machi, jeshi la Congo (FARDC) lilisitisha operesheni na zoezi la kupiga doria, ambazo jeshi hilo lilikua likiendesha na kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, katika Mkoa mzima wa Kivu-Kaskazini.
Jumanne usiku wiki hii, baada ya kupata taarifa ya shambulio hilo, jeshi la Congo liliwatuma wanajeshi wake wengi kwenye eneo la tukio.
Shambulio hilo linatokea ndani ya masaa 24 baada ya helikopta ya MONUSCO kushambuliwa. Mpaka sasa hakuna kundi lolote ambalo limekiri kuhusika na mashambulizi hayo. Umoja wa Mataifa unshuku kuwa mashambulizi hayo yametekelezwa na waasi wa Uganda wa ADF.
CHANZO: NA RFI
No comments:
Post a Comment