Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika Mashariki
amewataka mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama kufanya
mazungumzo nchini Burundi, Jumatano kabla ya mkutano wa viongozi wa
jumuia hiyo.
| Pierre Nkurunziza |
| Jakaya Kikwete |
Hii ni mara ya kwanza kwa jumuia hiyo kutuma ujumbe wa ngazi ya mawaziri kwenda Bujumbura katika jitihada za kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo ambayo kwa miaka mingi imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure alikuwa nchini Tanzania jana Jumatatu ambako alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.
Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Burundi kimesema watu wapatao kumi na wawili wameuawa tangu maandamano kuanza tarehe 26 Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake tawala cha CNDD-FDD kugombea katika uchaguzi wa Juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment