Pages

Tuesday, 5 May 2015

MTOTO MIAKA 8 AUAWA NA MBWA

Aisha Ally mwenye umri wa miaka 8 (pichani), mkazi wa Mtaa wa NSSF, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu  wa Shule ya Msingi ya St. Joseph, Dar, amefariki dunia baada ya kung’atwa na mbwa anayedaiwa kuwa na kichaa, Uwazi lina mkasa wote.
Aisha Ally akiwa hoi hospitali.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni nyumbani kwao Mbezi wakati mtoto huyo alipotumwa na mama yake mkubwa kwenda dukani kununua vocha ya simu.Akisimulia tukio zima kwa waandishi wetu, baba mzazi wa marehemu, Ally Ayub alisema:
“Siku ya tukio mwanangu alitumwa na mama yake mkubwa kwenda dukani kumnunulia vocha, sasa wakati anarudi nyumbani njiani alikutana na mbwa huyo akamshambulia kwenye mguu wa kushoto, mkono wa kushoto na mdomoni.
“Mwanangu alijitahidi kupambana naye ili kujiokoa lakini mbwa naye alikuwa na nguvu, akamng’ata sehemu hizo.”

“Baadhi ya watu waliokuwepo dukani waliona, wengine walianza kulia baada ya kumtambua mwanangu, wengine  walikimbilia eneo la tukio kwa lengo la kumwokoa, mmoja wao alimpiga teke yule mbwa akatokomea kusikojulikana.
“Ndipo yule mtu aliyempiga teke mbwa na watu wengine walimleta mwanangu nyumbani akiwa anavuja damu sehemu alizong’atwa. Niliumia sana! Na bado  nikikumbuka naendelea kuumia.”
Mzazi huyo alisema kwamba, kabla ya kumkimbiza hospitali Aisha, alimpaka dawa aina ya spiriti kwa lengo la kumkausha damu.Aliendelea kusema: “Baada ya hapo tulimkimbiza Hospitali ya Muhimbili, tulipokelewa vizuri lakini cha ajabu hata dawa aina ya yuso tuliambiwa tukanunue nje jambo lililotusikitisha sana.
“Shida kubwa ilikuwa ni mtoto wangu atibiwe hivyo jirani yangu aliyenisaidia gari pamoja na kunisindikiza, alikwenda kununua hiyo yuso, akapakwa na kuchomwa sindano moja, akafungwa majeraha kisha tukaambiwa turudi nyumbani na kupangiwa tarehe nyingine ya kurudi.”

No comments:

Post a Comment