Madrid ilishindwa kupindua matokeo ya kufungwa mabao 2-1 katika
mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Juventus baada ya kujikuta wakipata
sare ya bao 1-1 na kuwafanya mabingwa hao wa Serie kusonga mbele kwa
jumla ya mabao 3-2.
 |
| Carlo Ancelotti
|
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ancelotti amesema ni mapema mno kuzungumzia mustakabali wake kwani bado msimu haujamalizika.
Juventus
inatarajia kupambana na Barcelona katika mchezo wa fainali
utakaofanyika Juni 6 mwaka huu katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin,
Ujerumani.
Mara ya mwisho Juventus kutinga fainali ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 2003 wakati walipofungwa na AC Milan.
No comments:
Post a Comment