Hatua
hii inafuatia mtafaruku baina ya shirikisho la ligi kuu la Uhispania na
serikali ya taifa kuhusiana na ugavi wa mapato ya haki miliki ya
kupeperusha mechi. Pande zote zimeshindwa kukubaliana kuhusu ugavi wa mapato ya matangazo ya mechi za ligi hiyo maarufu duniani. Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa juma lijalo tarehe 16 mei.Marufuku hiyo itaathiri zaidi ya wachezaji laki sita (600,000) na mechi elfu thelathini (30,000).
Kufikia
hizi sasa Barcelona inaongoza jedwali la La Liga,wakiwa na alama mbili
pekee zaidi ya wapinzani wao wakuu Real Madrid huku zikiwa zimesalia
mechi tatu tu msimu ukamilike.
Serikali kuu imepitisha mswada mpya
ambao utasimamia ugavi wa fedha zinazotokana na hati miliki ya
matangazo ya mechi hizo za la Liga.
No comments:
Post a Comment