Bondia Kutoka Ufilipino Manny
Pacquiao amefanyiwa upasuaji wa bega lake alilodai kuwa ndiyo
iliyopelekea yeye kushindwa na Floyd Mayweather jumapili iliyopita.
Bondia huyo tayari anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.Hata hivyo daktari wake Neal ElAttrache, amesema kuwa amefurahia matokeo ya upasuaji huo licha ya ripoti kudokeza kuwa Pacquiao anahitaji muda wa mwaka mmoja kuuguza jeraha hilo.
NAC inapendekeza kushtakiwa kwa bondia huyo mfilipino kwani hakusajili maumivu ya aina yeyote katika fomu maalum siku moja kabla ya pigano.
Awali mwanadondi huyo alikuwa amesema yuko tayari kuzichapa dhidi ya Muingereza Amir Khan miongoni mwa wanandondi wengine.
No comments:
Post a Comment