Magazeti ya Afrika Kusini yanaripoti kuwa nchi hiyo ililipa dola milioni
10 kwa shirika la kandanda linaloongozwa na Jack Warner - mmoja kati ya
maafisa wa FIFA wanaotajwa katika tuhuma za rushwa.
Maafisa wa mashtaka wa Marekani wanasema malipo hayo hayakuwa halali -
na yalisaidia ombi la Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la
mwaka wa 2010. Lakini rais wa jumuia ya kandanda ya Afrika Kusini, Danny Jordaan, amekanusha hayo.
Maafisa ambao hawakutajwa majina, wanasema fedha hizo zilikusudiwa kuendeleza kandanda kati ya Waafrika wanaoishi uhamishoni. Na
BBC imekuja kujua kuwa mabenki mawili ya Uingereza yanachunguza matawi
yake kuhusu fedha katika mabenki hayo za maafisa wa FIFA.
Barclays
na Standard Chartered zilitajwa juma lilopita katika mashtaka ya
shirika la kuchunguza uhalifu la Marekani, FBI, dhidi ya maafisa wa
Shirikisho la Kandandana Duniani. Benki ya HSBC piya imetajwa. Babenki hayo hayakutuhumiwa kuwa yalifanya makosa.
Standard
Chartered ilisema inajua kuwa malipo mawili ya fedha yaliyopitishwa
katika benki hiyo yametajwa, na benki imesema inachunguza hayo. Barclays na HSBC zimekataa kusema kitu.
|
No comments:
Post a Comment