Mmoja wa makamanda wa ngazi za juu
katika jeshi la China ametetea hatua ya nchi hiyo za kuokoa ardhi kutoka
baharini katika maeneo yanayozozaniwa kusini mwa china.
Naibu Kamanda wa wanamaji wa China amemuambia
waziri wa usalama wa Marekani kuwa China haitasitisha mradi wake
Baharini
mradi wa kuokoa ardhi kutoka baharini.
Kauli
hiyo inawadia siku moja baada ya Marekani kutaka China isitishe mara
moja miradi hiyo ikidai kuwa inakiuka maadili ya jumuia ya mataifa
huru. Naibu amiri mkuu wa jeshi la wanamaji la China Su Jianguo
aliuambia mkutano mkuu nchini Singapore kuwa miradi huo unalengo la
kuboresha uwezo wa nchi yake kutekeleza majukumu yake ya kimataifa na
kusaidia eneo hilo.
Su Jianguo
Alisema kuwa kati ya majukumu hayo ni pamoja na jitihada za uokoaji, utunzi wa mazingira na uhuru wa safari za baharini. China inadai kuwa karibu eneo lote la kusini mwa bahari ya china ni lake. Nchi nyingi zinashuku kuwa miradi ina lengo la kuiwezesha China kudai kuwa maeneo makubwa kusini mwa bahari ya china.
Siku ya jumamosi, waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter aiitaka
Uchina isitishe mara moja mradi wa kuokoa ardhi kutoka baharini. Carter alisema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi.
Matamshi yake Carter yanafuatia taarifa ya makao makuu ya jeshi la
Marekani iliyodai kuwa Uchina imeweka silaha katika moja ya visiwa
hivyo.
Bwana Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi.
Hata hivyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment