Mahakama moja nchi Hispania imepiga
marufuku mgomo uliokuwa unaandaliwa na muungano wa wana soka nchini humo
ambao ulikuwa umepangwa kutekelezwa mwishoni mwa wiki hii.
Maamuzi ya mahakama hiyo yanatoa nafasi kwa pande zote mbili kuweka taratibu za namna ya kuutatua mzozo huo,ambao unatishia kuuzika mpira nchini humo na hata kuweka shaka ya kutooneshwa kwa mtanange baina ya timu mbili za Atletico Madrid na Barcelona.
Muungano huo wa wachezaji nchini Hispania, umesema kwamba serikali yao imejipanga kuweka mipango ya kisheria juu ya nini cha kufanya na kipi kisifanyike kuhakikisha kila klabu inalipa ushuru kuanzia vilabu vikubwa mpaka vya hadhi ya chini.
No comments:
Post a Comment