Mawaziri wa nchi za muungano wa
Ulaya wanakutana leo kuidhinisha mipango ya kuharibu mashua zinazotumiwa
kusafirisha wahamiaji kwenda Ulaya kutoka nchini Libya.
Viongozi wa Ulaya wanalenga kuchukua hatua kama hizo za kijeshi eneo la bahari la Libya na pwani ya Libya.
Karibu wahamiaji 6000 wanakadiriwa kuvuka bahari kutoka Afrika kaskazini na kuingia Ulaya mwaka huu.
No comments:
Post a Comment