Wahamiaji wa kabila la Rohingya waliookolewa na wavuvi
Wavuvi kutoka Indonesia wamesema
kuwa wameamriwa na Serikali kuwa wasiwalete wahamiaji wanaopatikana
wakielea kwenye vyombo baharini wasiokuwa na chakula au maji ya kutosha.
Baadhi ya wahamiaji waliookolewa na wauvuvi Indonesia
Maelfu ya wahamiaji wanadhaniwa kuwa wanaelea Baharini katika maeneo karibu na Indonesia, Thailand na Malaysia. Licha ya wito wa Umoja wa Mataifa kuwa wahamiaji waruhusiwe kufika
ufuoni, mataifa hayo matatu yamefukuza boti zilizojaa wahamiaji.
wavuvi wa Indonesia
Ni wale watu wanaojitahidi kufika nchi kavu pekee wanaoruhusiwa katika nchi hizo. Wahamiaji wengi ni Waislamu wa jamii ya Rohingya wanaotoroka mateso nchini Mynamar. Watu
wengi wanataka taifa la Myanmar kuchukua wajibu mkubwa zaidi kuhusiana
na wahamiaji hao lakini taifa hilo limekataa likidai kuwa halipaswi
kulaumiwa kwa hali hiyo.
No comments:
Post a Comment