Mratibu wa Mawasiliano na
uhamisishaji wa mradi wa Mama Ye unaoendeshwa na asasi ya Evidence for
Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID),
Chiku Lweno akielezea jitihada zinazofanywa na mradi wa Mama Ye katika
kukabiliana na vifo vya Mama na mtoto ambapo aliwataka waandishi wa
habari kutumia kalamu zao kuelemisha jamii ili iweze kuepukana na vifo
vya mama na mtoto ambalo nalo ni janga la taifa.
Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikali
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala akifafanua
jambo kwa washiriki wa mafunzo ya siku moja yaliyofadhiliwa na Shirika
la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) kuelekea kwenye kilele cha
sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani ambapo kitaifa
imefanyika mkoani Mara.
Mratibu wa Chama cha Wakunga
nchini (TAMA), Martha Rimoy akizungumzia nia ya chama hicho ni
kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa anapata huduma za
mkunga mtaalamu.
Afisa muuguzi mwandamizi kutoka
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini Manangwa akizungumzia
changamoto za upungufu wa wakunga, vituo vya kutolea huduma, dawa,
miundombinu n.k wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mjini
Musoma mkoani Mara.
Afisa wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) anayeshugulikia mifumo ya Afya, Felista
Bwana akitoa takwimu za nchi zinazoongoza kwa vifo vya mama na mtoto
kwenye mafunzo ya waandishi wa habari mjini Musoma.
Mwandishi wa habari wa gazeti la
The Citizen, mkoani Mara, Belina Nyakeke (katikati) akishiriki kwenye
mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika mjini Musoma na kufadhiliwa
na Shirika la UNFPA.
Mwandishi wa habari wa gazeti la
Tanzania Daima mjini Musoma, Igenga Mtatiro akiuliza swali kwa Afisa
muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini
Manangwa (hayupo pichani).
Pichani juu na chini ni baadhi ya
waandishi wa habari wa mkoani Mara ambao pia wanachama wa vilabu vya
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) walioshiriki mafunzo hayo
yaliyoratibiwa na Mradi wa Mama Ye kwa kushirikiana na UTPC na
kufadhiliwa na UNFPA.
Waandishi wa habari na wadau wakisikiliza kwa makini.
Waandishi wa habari na wadau wakisikiliza kwa makini.
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Rais wa Klabu za Waandishi wa
Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya (kushoto) akibadilishana mawazo
na Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy mara baada
ya kuhitimisha mafunzo hayo.
Na Mwandishi wetu, Musoma
SERIKALI imeshauriwa kuhakikisha sera na
mipango mizuri iliyopo kwa afya ya mama na mtoto mchanga inasimamiwa na
kutekelezwa ili kuliondoa taifa katika janga la kupoteza mama na watoto
wakati wa uzazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa
Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa Mama ye unaoendeshwa na asasi ya
Evidence for Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
Uingereza (DFID), Chiku Lweno katika mafunzo kwa waandishi wa habari
mjini Musoma.
Alisema bila kutekeleza mipango mizuri
ambayo Rais Jakaya Kikwete amekuwa championi wa masuala ya wanawake na
watoto kitaifa na mataifa, tatizo la vifo kwa wanawake wenye pingamizi
za uzazi na watoto wachanga.
Alisema kutokana na haja ya kutoa msukumo
katika masuala ya uzazi wameamua kuwapatia elimu waandishi wa habari ili
wawe chachu ya kutambua umuhimu wa ukunga na uzazi salama.
"Tunafunza waandishi wa habari ili waweze
kusukuma mbele shahuri hili ili kila mtu katika nafasi yake atetee
nafasi yake" alisema Lweno.
Alisema suala la mama na mtoto mchanga ni
masuala mtambuka ambapo mambo mengi lazima yaunganishwe yafikiriwe na
kutambuliwa ili kudhibiti vifo vya wanawake na watoto wachanga.
Alitaja masuala hayo kama upangaji wa
bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kusaidia kupatikana kwa wakunga
wataalamu na vifaa vyao vya kazi na maeneo ya kufanyia kazi. Aidha
kuwapo kwa ukubali wa wakunga na elimu ya uzazi.
Alisema ni vyema waandishi wa habari kama
watia chachu kuelimishwa mambo mengi yanayohusiana na uzazi salama
ambapo ndani yake kuna masuala ya bajeti na ufuaji wa wataalamu na
ufuatuiliaji wa sera na sheria zilizopo katika kuhakikisha usalama wa
mama na mtoto.
Alisema anaamini waandishi wa habari wakielewa mambo hayo watasaidia kukomaa nalo na kuwezesha kila mtu kuwajibika.
Naye Afisa Muuguzi mwandamizi kutoka Wizara
ya Afya na Ustawi wa jamii, Saturini Manangwa akiwasilisha mada kwa
waandishi wa habari alisisitiza haja za waandishi kutambua dhana ya afya
ya mama na mtoto kuwa ni kitu mtambuka kutokana na suala la lenyewe
kutegemeana.
Alisema serikali inapohimizwa kuwekeza kwa
mkunga kunatokana na ukweli kuwa huduma ya mama na mtoto mchanga
itakujwa bora kwa kuwa na mkunga bora mwenye vifaa na anayefahamu wajibu
wake kuanzia ujauzito wa mama hadi kujifungua kwake.
Alisema uwekezaji huo unagusia changamoto
nyingi zilizopo sasa kama upungufu wa wakunga, vituo vya kutolea huduma,
dawa, miundombinu na masuala anuai ambayo yameegemezwa na utambuzi wa
bajeti na umuhimu wake kama kipaumbele.
Alisema kwamba katika upangaji bajeti kila kitu kinategemea huwezi kusema unazidisha hiki na unakiacha hiki.
Alisema mathalani katika hali bora ya
ukunga na uwezo wa kumsaidia mhusika ,viwango vya dunia vilivyoweka na
Shirika la Afya Duniani (WHO) kila mkunga mmoja ahudumie angalau watu
sita, lakini sehemu kubwa ya dunia haifikii hivyo.
Aidha alisema kwa Tanzania kiwango ni
mkunga mmoja ahudumie watu 20-25 lakini kwa sasa Tanzania mkunga mmoja
anahudumia zaidi ya watu 50.
Kimsingi alisema Tanzania ina tatizo la
wakunga na pamoja na serikali kuanzisha vyuo vya kufunza wakunga na
kukubali mashirika ya dini nayo kufanya hivyo hali bado ni tete.
Hata hivyo alisema ni kupitia wakunga waliowataalamu upo uwezekano wa kuzuia vifo visivyo vya lazima.
Muuguzi huyo mwandamizi pia alisema katika
juhudi za serikali kunaanzishwa mafunzo ya mwaka mmoja ambapo yatatoa
maofisa afya ambao kazi yao kubwa itakuwa kujua idadi ya wanawake
wajawazito na wagonjwa katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa zahanati
iliyo karibu.
Alisema ofisa huyo kazi yake haitakuwa
hospitalini au kwenye zahanati bali kwenye jamii akitambua idadi ya
wagonjwa wake na kutoa taarifa sahihi ya hali ya afya ya kitongoji chake
kwenye zahanati.
Mmoja wa washiriki Belina Nyakeke ambaye ni
mwandishi wa habari wa magazeti alisema kwamba amefurahishwa na mafunzo
hayo ambayo yamempa nafasi ya kutambua wajibu wake katika kusaidia
kuondoa tatizo la vifo vya mama na mtoto mchanga.
Alisema japokuwa mafunzo ni ya muda mfupi lakini yamemfumbua macho kutambua wajibu na haki kwa wananchi na serikali.
Naye Ahmed Makongo akizungumzia mafunzo
hayo alisema yamemfanya atambue wajibu wake kusaidia kusukuma mambo
yaende sawa kwa upande wa waamuzi na pia wananchi husika kwa kuzingatia
mafunzo hayo yaliyoletwa kwao na Mama Ye na UTTPC chini ya Ufadhili wa
Shirika la Mpango wa watu Duniani (UNFPA)
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
No comments:
Post a Comment