Awali, Kiba alikaririwa akisema kuwa, mjengo huo wa kifahari ni wa ndugu yake aliyepo nje ya nchi ambaye alimpa ili aishi na ndugu zake (wa Kiba) wakati yeye (mmiliki) akiwa hayupo.Siku kadhaa mbele, baada ya Kiba kuvamiwa nyumbani hapo na watu kupora vitu huku akinusurika kuuawa, jamaa huyo alikaririwa redioni na kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa nyumba hiyo ni yake.
| Mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba. |
“Ninyi mnasema ule mjengo ni wa Ali (Kiba)? Acheni hizo, kwa taarifa yenu hiyo nyumba kapewa na mrembo f’lani hivi amazing, anaitwa Mariana, ni Mbongo anayeishi Singapore.
“Muulizeni huyo Kiba awaambie ukweli,” kilisema chanzo chetu kikisisitiza: “Hata Mariana aliposikia eti nyumba ni ya Ali (Kiba) alishangaa na akamaindi ile mbaya hivyo kwa sasa sidhani kama wanaelewana kwa ajili hiyo.”
Baada ya kukutana na mkanganyiko huo, gazeti hili lilimtafuta Kiba ambaye alikiri kwamba kweli nyumba hiyo siyo yake bali amepangisha huku akikana kusema kuwa anaimiliki.Alipoulizwa juu ya madai ya kupewa nyumba hiyo na mwanamke aitwaye Mariana, Kiba alisema hayo ni maneno tu kwani anachojua yeye amepangisha.
“Kwanza hebu nitumie picha nijue ni nyumba gani?” aliomba Kiba ambapo alitumiwa picha kwa WhatsApp ndipo akajibu:
“Okey, kama ni hiyo nimepangisha lakini siyo kwamba sina nyumba.”
No comments:
Post a Comment