PICHA ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayomuonesha akila mishikika uswahilini imezua gumzo la aina yake mitandaoni.
 |
| Staa wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akila mishikika uswahilini. |
Picha hiyo ambayo ilipigwa mwaka mmoja uliopita maeneo ya Tip Top,
Manzese jijini Dar, imeibua mjadala mpya juzikati kwenye mitandao ya
kijamii ambapo wengine walimpongeza kwa kitendo hicho wengine wakisema
si cha hadhi yake.
 |
| Nasibu Abdul ‘Diamond’. |
“Hii ni nzuri kwa mtu kama Diamond akila
uswahilini. Anaonesha siyo mtu wa majivuno,” alichangia mdau mtandaoni
huku wengine wakidai si sawa kwani anajiabisha.
Baada ya chanzo hicho kuipata picha hiyo na kumtumia mwandishi wetu,
Mikito Nusunusu ilimtafuta Diamond ili aweze kuizingumzia lakini simu
yake haikupatikana lakini Bab Tale alipatikana na kukiri maelezo ya
chanzo chetu.
“Hakukuwa na ishu zaidi ya kuitamani mishikaki, tukaona tununue, mbona ni ya toka mwaka jana?,” alisema Bab Tale.
No comments:
Post a Comment