| Kyoko Hamada katika mizunguko yake kama bibi kizee. |
Hamada, ambaye ni mzaliwa wa Tokyo, Japan aliamia nchini Marekani akiwa na miaka 15 na alipata wazo hilo baada ya kujitolea kutembelea makazi ya wazee wanaoishi maisha ya upweke.
Baada ya hapo aliamua kuanza mradi aliouita jina la 'I Used To Be You' ambapo alikuwa akizunguka mitaa ya New York kama bibi kizee na kupiga picha zake tangu mwaka 2012 na ameandaa kitabu cha picha chenye kurasa 99 ambacho atakichapisha.
| Picha za Kyoko Hamada kabla na baada ya kujifanya bibi kizee. |
Mama huyo anaeleza kuwa wakati mwingine watu walikuwa wakifungua milango kwa ajili ya kumsaidia huku wengine wakimsaidia mizigo yake mizito ila jambo la kushangaza alilojifunza ni kwamba hakuna mtu aliyeonyesha kumjali au kumtambua.
Zifuatazo ni picha za Hamda katika mradi wake huo:
No comments:
Post a Comment