Pages

Tuesday, 19 May 2015

Saratani:Mwanaharakati ajifunga nyororo

Mwanaharakati David Ndung'u Wanjohi wa Ol Kalau kaunti ya mkoa wa kati nchini Kenya amejifunga nyororo katika chumba cha dharura cha hospitali kuu ya Kenyatta Jijini Nairobi na kuanza mgomo wa kutokula ili kupinga kile alichokitaja kama ukosefu wa vifaa vya kuwasaidia wagonjwa wengi wa ugonjwa wa saratani nchini.
david Ndung'u Wanjohi
David ambaye ni baba wa watoto wawili amesema kuwa serikali na jamii kwa jumla inapaswa kutoa raslimali zilizopo kununua vifaa vya tiba kwa wagonjwa ambao wanangojea tiba hadi mwaka 2017.
Mwanaharakati aanza mgomo wa kutokula ili kuishinikiza jamii na serikali kununua vifaa zaidi vya tiba ya saratani

No comments:

Post a Comment